Rais wa China ahutubia mkutano usio rasmi wa 29 wa viongozi wa APEC
2022-11-18 14:52:20| CRI

Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano usio rasmi wa 29 wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) uliofunguliwa leo asubuhi huko Bangkok, Thailand.

Kwenye hotuba yake rais Xi amesema, katika miongo kadhaa iliyopita, ushirikiano wa uchumi kati ya nchi za Asia na Pasifiki umeendelea vizuri, na kufanya “muujiza wa Asia na Pasifiki” unaoishangaza dunia, na kuongeza kuwa, kutokana na hali mpya ya dunia, nchi za eneo hilo zinapaswa kushirikiana kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja.

Rais Xi ametoa mapendekezo manne ya kujenga eneo la Asia na Pasifiki, ambayo ni kulinda haki ya kimataifa na kujenga eneo la Asia na Pasifiki lenye amani na utulivu, kushikilia moyo wa kufungua mlango na kushirikisha na kujenga kwa pamoja eneo la Asia na Pasifiki lenye utajiri, kushirikilia njia ya kijani ya kujiendelea na kujenga eneo la Asia na Pasifiki lenye usafi kuvutia, na kushirikilia jumuiya yenye hatma ya pamoja na kujenga eneo la Asia na Pasifiki la kusaidiana.