China Media Group yaandaa seminar na wadau wa habari wa Afrika
2022-11-18 20:45:31| cri

Semina yenye jina la "China na Dunia Kuanza Safari Mpya" imeandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji wa China, China Media Group (CMG), ilifanyika Jumatano huko Nairobi.

Maofisa waandamizi wa wapatao sitini kutoka vyombo vya habari, wataalam na wasomi kutoka nchi 20 za Afrika wamechangia ufahamu wao kuhusu jinsi ya kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja. Semina hiyo ni sehemu ya shughuli za mwisho wa mwaka kuhusu ushirikiano kati ya China na vyombo vya habari vya Afrika, ambayo pia imeambatana na uzinduzi wa vipindi vya televisheni ya kimataifa ya China CGTN vitakavyozingatia maendeleo ya Afrika.

Wahariri na wasimamizi mbalimbali wa vyombo vya habari kati ya China na nchi zilzioshiriki wametoa mwito wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya China na Afrika, ili kuepusha upotoshaji wa vyombo vya habari va nchi za magharibi, na utegemezi wa vyombo vya habari vya magharibi.