Semina ya vyombo vya habari vya China na Afrika ya “China na Dunia katika Safari Mpya” yafanyika Nairobi
2022-11-18 10:19:23| CRI

Semina ya vyombo vya habari vya China na Afrika yenye kauli mbiu ya “China na Dunia katika Safari Mpya” imefanyika Nairobi, Kenya, ikiandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Afrika.

Wasimamizi wa vyombo vya habari na wataalam 60 kutoka nchi 20 za Afrika zikiwemo Kenya, Rwanda, Tanzania, Madagascar, Sudan Kusini, Zambia na Sierra Leone wamefanya majadiliano ya kina juu ya ajenda kama “China katika safari mpya ina maana gani kwa Afrika” “safari mpya ya kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika inakwenda wapi” na “ushirikiano wa vyombo vya habari vya China na Afrika utaleta nini kwa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya pande hizo mbili”. Washiriki wamekubaliana kuwa maendeleo mapya baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China yatatoa fursa mpya kwa Afrika, na pia ni injini mpya kwa ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika, na kwamba ushirikiano wa vyombo vya habari vya China na Afrika una nguvu kubwa ambazo hazijatumiwa ipasavyo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Sera ya Afrika nchini Kenya Profesa Peter Kagwanja amesema kwenye hotuba yake kuwa China inatafuta maendeleo kwa amani, kitu ambacho kinaendana na maslahi ya watu wengi. Afrika na China zote zina ustaarabu wenye historia ndefu, zote zilikuwa na historia ya kuteswa na nchi za magharibi, na zote zinakabiliwa na suala la maendeleo. Nchi za magharibi ziliwahi kuiita Afrika kama “bara lisilo na matumaini”, na kwa kupitia kushirikiana na China, Afrika inapata matumaini. Afrika itanufaika na safari mpya na maendeleo mapya ya China.