Peng Liyuan atembelea taasisi ya muziki Bangkok
2022-11-19 22:38:27| cri

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China leo Jumamosi alitembelea Taasisi ya Muziki ya Binti Mfalme Galyani Vadhana huko Bangkok, Thailand.

Peng alikaribishwa kwa furaha na Naraporn Chan-o-cha, mke wa Waziri Mkuu wa Thailand Prayut Chan-o-cha, waziri wa elimu ya juu, sayansi, utafiti na uvumbuzi wa Thailand Anek Laothamatas, pamoja na maofisa waandamizi wa Taasisi hiyo.

Peng akiwa ameongozana na Naraporn, alitazama maonyesho yaliyofanywa kwa pamoja na taasisi hiyo na Chuo Kikuu cha Sanaa cha Nanjing cha China.

Peng alipongeza maonyesho hayo kabla ya kutoa shukrani zake kwa binti mfalme marehemu Galyani Vadhana kwa kutetea kuanzishwa kwa taasisi hiyo inayojitolea kutoa mafunzo kwa vipaji vya hali ya juu vya muziki. Pia alitoa shukrani kwa Naraporn kwa kukuza ushirikiano kati ya taasisi hiyo na vyuo vya China.

Peng alisema muziki hauna mipaka, na kwamba ingawa mataifa hayo mawili yana lugha tofauti, muziki unaweza kutumika kama kifungo kati ya mioyo ya watu wao, akiongeza kuwa anahisi China na Thailand ziko karibu kama familia moja kwenye maonyesho hayo.