Xi na Prayut wakubaliana kujenga jumuiya ya China na Thailand yenye mustakabali wa pamoja iliyo imara, yenye ustawi na endelevu zaidi
2022-11-19 22:39:40| cri

Rais Xi Jinping wa China na Waziri Mkuu wa Thailand Bw. Prayut Chan-o-cha leo Jumamos walikubaliana kujenga jumuiya ya China na Thailand yenye mustakabali wa pamoja iliyo imara, yenye ustawi na endelevu zaidi.

Kwenye mazungumzo na Bw. Prayut, Rais Xi alisema China inapenda kuendeleza urafiki wa kipekee kati ya China na Thailand, ambao ni "karibu kama familia moja," kuingiza maana mpya katika urafiki huo, na kufungua ukurasa mpya wa zama hizi katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wao.

Amesema China iko tayari kuimarisha mshikamano na ushirikiano na Thailand na nchi nyingine za Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN), na kujenga kwa pamoja“nyumba” yenye amani, usalama, ustawi, nzuri na amani, ili kuendelea kuibua vichochezi vipya vya ukuaji wa uchumi kwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na ASEAN.

Kwa upande wake, Bw. Prayut alipongeza kufanyika kwa mafanikio kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na rais Xi Jinping kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC. Amesema ziara ya Xi nchini Thailand na kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Kiuchumi wa APEC ni ziara yake ya kwanza nchini Thailand tangu awe rais wa China, ambayo ina umuhimu mkubwa.

Ameongeza kuwa Thailand inaunga mkono Pendekezo la Maendeleo ya Dunia  na Pendekezo la Usalama Dunia , lililotolewa na Xi na kuiunga mkono China katika kubeba jukumu kubwa katika masuala ya kikanda na kimataifa.