Nchi za Afrika Magharibi zajadili kuandaa kikosi cha dharura kudhibiti waasi
2022-11-21 08:50:14| CRI

Nchi saba wanachama wa Pendekezo la Accra zinajadili uundwaji wa kikosi cha dharura cha kijeshi kitakaposhughulika na makundi ya waasi yenye silaha katika kanda hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Usalama wa Taifa wa Ghana, Albert Kan Dapaah, alipokutana na wanahabari ili kutoa taarifa ya maendeleo yaliyofikiwa katika kulinda mamlaka na ardhi ya nchi wanachama wa Pendekezo hilo na kanda hiyo kwa ujumla.

Amesema mipaka isiyo rasmi katika kanda hiyo na maeneo yasiyosimamiwa katika nchi kadhaa ni baadhi ya vivutio kwa makundi ya waasi yenye silaha na wapiganaji wa Jihadi. Ameongeza kuwa, moja ya hatua muhimu ni kuhakikisha kuwa hakuna maeneo mengi ya mpaka yasiyo na usimamizi katika nchi wanachama, na pia kuchukua hatua zitakazoweka ugumu kwa wapiganaji wa Jihadi kuwafanya vijana wa maeneo ya mpakani kuwa na msimamo mkali.