Guinea ya Ikweta yafanya uchaguzi wa rais, wabunge na serikali za mitaa
2022-11-21 08:41:58| cri

Guinea ya Ikweta jana imefanya uchaguzi wa rais, wabunge na serikali za mitaa.

Zoezi la kupiga kura katika uchaguzi huo lilianza saa mbili asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni, na watu zaidi ya 400,000 walijiandikisha kupiga kura kote nchini humo.

Aidha, takriban madiwani 600 wa serikali za mitaa watachaguliwa katika uchaguzi huo.