Xi apongeza Tokayev kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Kazakhstan
2022-11-21 20:31:46| cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya kumpongeza Kassym-Jomart Tokayev kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Kazakhstan, akisema matokeo haya yameonyesha vya kutosha  imani na uungaji mkono wa watu wa Kazakhstan kwa Tokayev.

Rais Xi amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kazakhstan, na yuko tayari kufanya juhudi pamoja na rais Tokayev na kutumia maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi mbili kama mwanzo mpya, kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa kudumu wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Kazakhstan, na kujenga jumuiya ya China na Kazakhstan yenye mustakabali wa pamoja ili kunufaisha nchi na watu wake.