Rais wa Uganda asema EAC inafanya kazi kurejesha amani nchini DRC
2022-11-21 08:46:46| CRI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema nchi za Afrika Mashariki zinafanya kazi pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kurejesha amani katika eneo la mashariki mwa DRC.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Uganda imesema, rais Museveni amesema hayo alipokutana na ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliokuwa ziarani nchini humo. Amesema wakati mazungumzo kati ya makundi ya DRC yatapewa kipaumbele, nguvu itatumika dhidi ya makundi yatakayoendeleza mapigano.

Kuhusu tuhuma kuwa baadhi ya nchi jirani zinatoa silaha kwa kundi la waasi la M23, rais Museveni ameuambia ujumbe huo kuwa Afrika Mashariki haitashindwa kupeleleza suala hilo na kujua ukweli.

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uko nchini Uganda baada ya kumaliza ziara kama hiyo nchini DRC na Rwanda.