Mkutano wa COP27 wamalizika kwa kufikia makubaliano ya kuanzisha mfuko wa hasara na uharibifu
2022-11-21 08:53:36| CRI

Mfumo wa “Hasara na Uharibifu” uliosubiriwa kwa muda mrefu ili kuzisaidia nchi zilizo hatarini kutokana na mabadiliko ya tabianchi umeidhinishwa jana jumapili wakati Mkutano wa 27 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Pande Zilisoaini Makubaliano ya Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) ulipomalizika mjini Sharm El-Sheikh nchini Misri.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika taarifa yake kuwa, anapongeza kuanzishwa kwa mfuko huo na utekelezaji wake katika kipindi kijacho.

Akizungumza katika hafla ya ufungaji wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye pia ni rais wa COP27 Sameh Shoukry amesema, mafanikio ya mkutano huo yanatoa ujumbe kwa dunia kuwa diplomasia ya pande nyingi bado inafaa, na kwamba licha ya matatizo na changamoto, bado jamii ya kimataifa inaungana kupambana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Naye kiongozi wa ujumbe wa China katika mkutano wa COP27 Zhao Yingmin ambaye pia ni naibu Waziri wa Ikolojia na Mazingira amesema, mkutano huo umepata maendeleo katika mabadiliko, ufadhili, na “hasara na uharibifu”, ambayo ni masuala yanayoleta wasiwasi mkubwa kwa nchi zinazoendelea.