Rais wa Cuba kufanya ziara nchini China kuanzia tarehe 24 hadi 26, Novemba
2022-11-21 20:30:46| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying leo ametangaza kuwa, katibu wa kwanza wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Cuba ambaye pia ni  rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel atafanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia tarehe 24 hadi 26, Novemba  kutokana na mwaliko wa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na rais wa China Xi Jinping.