Tanzania yasindika tani 70,000 za korosho katika mwaka 2022
2022-11-21 08:55:12| CRI

Makamu wa rais wa Tanzania Dr. Philip Mpango hivi karibuni amesema, Tanzania ilisindika tani 70,000 za korosho katika mwaka 2022.

Dr. Mpango amesema hayo aliposhiriki kwenye sherehe ya kutoa tuzo kwa watengenezaji hodari wa nchi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa niaba ya rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Amesema hii ni hatua sahihi ya kuongeza thamani kwa mazao ya kiuchumi, na kuongeza kuwa, idadi hiyo imeongezeka kwa mara moja kuliko tani 34,000 ya mwaka 2021.