Naibu mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China ahudhuria mkutano wa kutangaza matokeo ya awali ya kampeni ya "Kampuni Mia, Vijiji Elfu"
2022-11-22 11:54:20| CRI

Naibu mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masuala ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Yu Yong, alihudhuria mkutano na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya awali ya kampeni ya "Kampuni Mia, Vijiji Elfu" na mkutano wa kilele wa wajibu wa kijamii wa kampuni za China barani Afrika.

Bw. Yu Yong alisema kampeni hiyo ni hatua muhimu yenye ubunifu kati ya “Miradi Tisa” ya ushirikiano wa China na Afrika iliyotangazwa na rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC), ambayo inalenga kuunganisha utekelezaji wa wajibu wa kijamii wa kampuni za China barani Afrika na ushirikiano wa kupunguza umasikini kati ya pande hizo mbili na kuhimiza maendeleo endelevu katika jamii ya Afrika.

Amesema anatarajia kuwa China na Afrika zitashirikiana zaidi kupitia kampeni hiyo kuendeleza tasnia za kupunguza umaskini, kusaidia kuandaa wafanyakazi wa kiufundi, kutimiza maingiliano chanya kati ya makampuni ya China na wenyeji na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya.