Baraza la Uchumi na Biashara la China na Afrika la mwaka 2022 lafanyika mjini Jinhua
2022-11-22 08:50:57| cri

Baraza la Uchumi na Biashara la China na Afrika la mwaka 2022 limefanyika jana mjini Jinhua, mkoani Zhejiang, ambapo mada kuu ya baraza hilo ni "mfungamano kati ya watu, kujifunza kwa utamaduni kutoka kwa kila mmoja na ushirikiano wa kunufaishana".

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda na Biashara la China, Bw. Gao Yunlong amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika umepata matokeo mazuri. Katika mwanzo mpya wa kihistoria, anatumaini pande hizo mbili zitaendelea kuzingatia uvumbuzi na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya hali ya juu ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yao.