Rais Xi Jinping wa China atoa salamu za pole kwa rais Joko Widodo wa Indonesia kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo
2022-11-22 20:37:14| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pole kwa rais Joko Widodo wa Indonesia kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo.

Katika salamu hizo rais Xi kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, pia ametoa salamu za pole kwa wafiwa na familia zao.

Amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wa rais Widodo na serikali yake, wananchi walioathiriwa watashinda maafa na kujenga upya makazi yao.