Mjumbe mpya wa AU atoa wito wa umoja katika kupambana na ugaidi nchini Somalia
2022-11-22 08:31:28| CRI

Mjumbe mpya wa Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Afrika (AU) nchini Somalia Mohammed El-Amine Souef, ametoa wito wa umoja na uvumbuzi katika kupambana na ugaidi nchini humo.

Bw. Soef, ambaye pia ni mkuu wa Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) amesema, atafanya kazi pamoja na pande mbalimbali na wadau husika kutimiza jukumu la Tume hiyo katika kuboresha utulivu wa kisiasa na usalama nchini humo. 

Soef amerejea tena kuwa lengo la Tume hiyo nchini Somalia ni kuunga mkono serikali ya Somalia katika kujenga nchi tulivu na salama, na kutoa mchango katika maelewano ya kijamii, upatanishi na ujenzi wa uwezo.