Kenya yaunda timu ya kudhibiti athari za ukame nchini humo
2022-11-22 08:30:47| CRI

Rais wa Kenya William Ruto ameunda kamati ya watu 15 ya sekta binafsi itakayosaidia kukabiliana na ukame unaoikumba nchi hiyo.

Katika tangazo la serikali lililotolewa jana jumatatu, rais Ruto amesema timu hiyo itasaidia juhudi za serikali katika kupunguza athari za ukame, na kuongeza kuwa, kamati hiyo itashughulika na masuala mengine ikiwa ni pamoja na program za uhamishaji wa fedha ili kulinda jamii dhidi ya athari za ukame. Amesema Kenya, kama nchi nyingine za Pembe ya Afrika, inakabiliwa na uhaba wa mvua unaosababisha ukame na mavuno duni.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Kusimamia Ukame ya Kenya, zaidi ya watu milioni 4 wanakabiliwa na uhaba wa chakula nchini Kenya, hususan katika maeneo kame na nusu kame.