UNECA yasema mageuzi ya viwanda ni muhimu kwa mabadiliko endelevu ya Afrika
2022-11-22 08:29:56| CRI

Kaimu katibu mkuu wa Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Antonio Pedro amesema, mageuzi endelevu barani Afrika yanahitaji mageuzi endelevu ya kiviwanda yanayoweza kuvumilia changamoto za kimataifa.

Bw. Pedro amesema hayo katika Siku ya Mageuzi ya Viwanda barani Afrika inayoadhimishwa kila Novemba 20. Amesisitiza kuwa mageuzi ya viwanda ni muhimu kwa Afrika kwa kuwa bidhaa za msingi, za kilimo ama zingine, zinachukua asilimia kubwa ya mauzo ya nje ya Afrika kwa dunia, huku bidhaa zilizotengenezwa zinachukua asilimia kubwa ya bidhaa zinazoagizwa nje ya bara hilo.

Amesema kuongeza thamani ya malighafi zinazopatikana ndani ya bara hilo kutafanya rasilimali zilizopo Afrika kuwa baraka, badala ya kuendelea kuwa mzigo.