Rais wa China atuma salamu za rambirambi kwa rais wa Indonesia kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Indonesia
2022-11-23 08:10:42| cri

Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Indonesia Joko Widodo kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Jumatatu magharibi mwa Indonesia.

Katika salamu zake, rais Xi ameeleza kusikitishwa kwake na uharibifu na hasara kubwa  za mali kutokana na tetemeko hilo, na kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali na watu wa China, kwa familia za watu waliofariki dunia na waliojeruhiwa katika tetemeko hilo.

Rais Xi pia amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wa rais Widodo na serikali ya Indonesia, watu waishio katika maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi watashinda taabu na kujenga upya maskani yao .

Idara ya Kitaifa ya Kudhibiti Majanga nchini Indonesia imesema jana Jumanne kuwa, idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko hilo imefikia watu 268 na wengine 151 bado hawajajulikana  walipo.