Sudan Kusini na IMF zafikia makubaliano rasmi ya fedha za dharura dola milioni 112.7 za kimarekani
2022-11-23 08:08:06| cri

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na serikali ya Sudan Kusini zimefikia makubaliano rasmi ya kutoa msaada wa dharura wa dola za kimarekani milioni 112.7 chini ya Dirisha jipya la Chakula ambazo zitaisaidia nchi hiyo kukabiliana na ukosefu wa usalama wa chakula, kusaidia matumizi, na kuboresha akiba ya fedha za kigeni.

Katika taarifa yake, IMF imesema mamlaka nchini Sudan Kusini zimeahidi kufanya uratibu na wenzi wa kuaminika wa maendeleo ili kutoa dola za kimarekani milioni 20 kutoka mfuko wa Mkopo wa Dharura (RFC) zitakazoingizwa katika mifumo iliyopo kutoa msaada wa dharura wa kibinadamu ili kusaidia kukabiliana na uhaba wa chakula.