Tanzania yagawa chakula kwa sehemu zinazokabiliwa na uhaba wa chakula
2022-11-23 08:06:12| cri

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Hussein Bashe amesema, serikali ya nchi hiyo imetoa msaada wa chakula kwa wilaya 41 zinazokabiliwa na uhaba wa chakula nchini humo.

Amesema kutokana na kupanda kwa bei za vyakula kunakosababishwa na ukame wa muda mrefu, serikali imesambaza chakula kwenye wilaya hizo ambacho kitauzwa kwa bei nafuu, na amesisitiza kuwa serikali ina akiba ya kutosha ya chakula.

Novemba 11, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa aliwataka Watanzania kuweka akiba ya chakula kutokana na nchi hiyo kukumbwa na ukosefu wa mvua na ukame wa muda mrefu.