Watu 17 wafariki katika ajali ya barabarani nchini Nigeria
2022-11-23 08:09:56| cri

Watu 17 wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea jana jumanne pembezoni mwa mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Msemaji wa Jeshi la Usalama Barabarani nchini humo Bisi Kazeem amesema katika taarifa yake kuwa, ajali hiyo ilihusisha lori na basi la abiria, na ilitokea katika barabara kuu ya Kwali-Abaji karibu na eneo la Awawa mjini Abuja.

Amesema uchunguzi wa awali umeonesha kuwa, ajali hiyo ilisababishwa na mwendo wa kasi na uchovu.