Watu 26 wafariki kutokana na Homa ya dengue nchini Sudan
2022-11-24 08:53:30| CRI


 

Mkuu wa Idara ya hali ya dharura ya afya na udhibiti wa majanga katika Wizara ya Afya ya Sudan Montasir Mohamed Osman amesema, watu 26 wamefariki kutokana na homa ya dengue nchini humo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Bw. Osman amesema kesi 462 zimethibitishwa kuwa na homa hiyo, na kesi nyingine 3,439 zinashukiwa za homa ya dengue nchini humo.

Wizara ya Afya nchini Sudan imechukua hatua zinazohitajika kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwemo kupeleka timu kukabiliana na ugonjwa huo, kutoa dawa na damu, kufanya ufuatiliaji na uchunguzi wa kila siku, na pia kutoa namba ya mawasiliano kwa ripoti za maambukizi na kesi zinazoshukiwa.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa kesi 1,068 za homa ya dengue zimeripotiwa nchini Sudan tangu mwezi Oktoba.