Rais wa Zimbabwe ahutubia bunge la nchi hiyo
2022-11-24 08:54:30| CRI

Rais wa Zimbabwe ahutubia bunge la nchi hiyo

 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa jana jumatano alilihutubia bunge la nchi hiyo katika ukumbi mpya wa bunge uliojengwa kwa msaada wa China.

Katika hotuba yake, rais Mnangagwa aliishukuru China kwa kutoa fedha na kujenga jengo la Bunge katika eneo la Mlima Hmpden, kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.

Jengo hilo ambalo fedha na ujenzi wake ni zawadi ya China kwa Zimbabwe, ni moja ya matokeo ya ushirikiano kati ya China na Afrika unaolenga kuimarisha urafiki na mshikamano kati ya watu wa Zimbabwe na China.