Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei ya Marekani yasababisha malalamiko kutoka kwa Ulaya
2022-11-24 12:20:56| CRI

Rais Joe Biden wa Marekani alisaini Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei mnamo mwezi Agosti mwaka huu, ambayo inaruhusu serikali ya Marekani kutoa ruzuku kubwa kwa viwanda vya magari ya umeme yanavyotengenezwa nchini humo, hatua ambayo imesababisha malalamiko kutoka kwa nchi za Umoja wa Ulaya (EU).

Waziri wa Uchumi na Fedha wa Ufaransa Bw. Bruno Le Maire na Naibu Waziri mkuu wa Ujerumani Bw. Habeck wamefanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Paris. Bw. Le Maire amesema serikali za Ufaransa na Ujerumani zimekubaliana kuwa zinapaswa kujibu vikali Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei wa Marekani, na EU lazima itetee maslahi yake.

Rais Macron wa Ufaransa amewashawishi wafanyabiashara wa Ulaya waendelee kubaki Ulaya na kuiwekeza Ulaya.

Gazeti la "Financial Times" la Uingereza limesema kwamba hatua ya ruzuku ya Biden ni ishara ya hatari, inayozilazimu nchi za Ulaya kuwa macho.