China yapenda kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja katika anga ya juu
2022-11-24 08:53:52| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, China inapenda kushirikiana na nchi zote zinazojikita katika matumizi ya amani ya anga ya juu ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja katika anga ya juu ili kuwezesha ustaarabu wa binadamu kuelekea kwenye nafasi pana zaidi.

Bw. Zhao amesema, anga ya juu na uchunguzi wake ni kazi ya pamoja ya watu wote, na China siku zote inasisitiza kufanya ushirikiano katika utafiti wa anga ya juu kwa msingi wa usawa, kunufaishana, matumizi ya amani na maendeleo shirikishi.