Baraza la Usalama la UM laomba kuondolewa kwa waasi wa M23 nchini DRC
2022-11-24 08:55:50| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kusimamishwa mara moja kwa mapigano na vitendo vingine vinavyofanywa na kundi la waasi wa M23, na kulitaka kuondoka katika maeneo yote linayoyakalia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika taarifa yake, Baraza hilo limelaani vikali kuanza upya kwa mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo mkoani Kivu Kaskazini kuelekea mji wa Goma na maeneo mengine nchini DRC, na kuwalaumu waasi hao kwa kufanya hali ya usalama na utulivu katika eneo hilo kuwa mbaya zaidi na kuongeza mgogoro wa kibinadamu.

Nchi wajumbe wa Baraza hilo wameeleza wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa wakimbizi wa ndani na watu wakimbizi, na kutoa wito kwa pande zote, hususan kundi la M23, kuruhusu mahitaji ya lazima ya kibinadamu kuwafikia walengwa, na pia kujizuia kufanya mashambulizi dhidi ya raia