Watu watano wa familia moja wauawa kwenye shambulizi la risasi katika msikiti huko Kabul
2022-11-24 10:17:09| cri

Msemaji wa polisi wa Kabul, Khalid Zadran, jana amethibitisha kuwa, watu watano wa familia moja wameuawa na mwingine mmoja kujeruhiwa kwenye shambulizi la risasi lililotokea ndani ya msikiti mmoja katika mji huo mkuu wa Afghanistan.

Zadran amesema, jana asubuhi mtu mmoja aliyekuwa na bunduki alifyatua risasi kwa watu waliokuwa wakisali ndani ya msikiti wa Kabul, na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja.

Zadran ameongeza kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha huenda uadui ndio chanzo cha shambulizi hilo.