Kampuni ya China nchini Zambia yawapatia wafanyabiashara wa chakula sehemu safi na salama kuuza bidhaa zao
2022-11-24 11:07:23| CRI

Kipindi cha Daraja kinachokujia kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kinakufahamisha mambo mbalimbali kuhusu uhusiano, ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika. Katika kipindi cha leo, licha ya habari za wiki hii zilizohusisha China pamoja na nchi za Afrika, tutakuwa na ripoti kuhusu kampuni ya China nchini Zambia kuwapatia wafanyabiashara wa chakula sehemu safi na salama kuuza bidhaa zao, pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi.