Angola: DR Congo na Rwanda zakubaliana kusitisha mapigano katika mazungumzo
2022-11-25 11:51:12| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Bw. Tete Antonio, amesema Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimefikia makubaliano ambayo yanaweza kumaanisha kupitishwa kwa usitishwaji vita katika eneo linalokumbwa na ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Rais Felix Tshisekedi wa DRC alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta mjini Luanda, wakati hali ya wasiwasi ikiongezeka kati ya majirani hao huku kukiwa na mapigano kwenye mpaka wa nchi zao.

Eneo la mashariki mwa DRC limeshuhudia mapigano makali katika miezi ya hivi karibuni kati ya wanajeshi wa Kongo na kundi la waasi la M23. Bw. Tete amesema makubaliano hayo yalifikiwa ili kusitisha mapigano mara moja.

Mapigano hayo yamezua mvutano wa kidiplomasia, huku DRC ikiishutumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi, jambo ambalo Rwanda inakanusha.