UNOCHA yaonya kuhusu mlipuko wa kipindupindu nchini Ethiopia
2022-11-25 08:28:01| cri

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Binadamu (UNOCHA) imeonya juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kusini mashariki mwa Ethiopia, wakati kesi 491 za kipindupindu ikiwemo vifo 20 vikiripotiwa kufikia sasa.

UNOCHA imesema, mlipuko wa kipindupindu umeenea katika vijiji 41 vya wilaya 4 katika ukanda wa Bale wa mkoa wa Oromia, na wilaya 2 za ukanda wa Liban wa mkoa wa Somali.

Taasisi ya Afya ya Umma ya Ethiopia (EPHI), mamlaka za afya za mikoa ya Oromia na Somali, Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) na wadau wengine wameongeza juhudi za kuimarisha afya, usafi na huduma ya vyoo katika maeneo yaliyopewa kipaumbele.