Sekta ya utengenezaji nchini China yavutia uwekezaji wa kigeni
2022-11-25 09:05:42| cri

Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bi. Shu Yuting amesema, mwaka huu sekta ya utengenezji inaendelea kuvutia uwekezaji wa kigeni.

Bi. Shu amesema, kampuni nyingi za kigeni zina imani na China ambayo ina fursa kubwa za soko, mfumo bora wa viwanda, miundombinu mizuri, na mazingira ya jamii yenye utulivu, mambo ambayo yameongeza nguvu ya uwekezaji kwa China, na miradi mingi iliyowekezwa na kampuni za kigeni imejengwa.

Mwaka 2021 sekta ya utengenezji nchini China ilivutia uwekezaji wa kigeni wa dola za kimarekani bilioni 33.73, na kuongezeka kwa asilimia 8.8 kuliko mwaka 2020.