Mazungumzo ya pili kati ya vijana wa China na Afrika yafanyika kwa njia ya video
2022-11-28 08:57:44| CRI


 

Mazungumzo ya pili ya vijana wa China na Afrika yaliyoandaliwa na Shirikisho la Urafiki wa Watu wa China na Nchi za Nje la China yamefanyika kwa njia ya video, na kuwashirikisha wajumbe 300 kutoka China na nchi 35 za Afrika. 

Naibu mkuu wa Shirikisho hilo Jiang Jiang amesema, historia na hali ya hivi sasa zote zimethibitisha kuwa, uhusiano kati ya China na Afrika umeanzishwa kwa pamoja na watu wa pande hizo mbili. Amesisitiza kuwa, vijana ni mustakabali wa nchi, na vijana wa China na Afrika ni mustakabali wa urafiki kati ya pande hizo mbili.

Balozi wa Senegal nchini China Ibraima Sira amepongeza uzoefu wa China katika kupunguza umaskini, na kusema inapaswa kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ambayo kiini chake ni vijana wa Afrika na China.