Rais wa Guinea ya Ikweta ashinda katika uchaguzi mkuu
2022-11-28 09:41:33| CRI

Matokeo ya kura za uchaguzi yaliyotangazwa kupitia tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Guinea ya Ikweta yameonyesha kuwa, rais wa sasa wa nchi hiyo Teodoro Obiang Nguema Mbasogo ameshinda uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 mwezi huu kwa kupata asilimia 94.9 ya kura zote zilizopigwa, na ataendelea na urais wake kwa muhula mwingine wa miaka saba.

Matokeo hayo pia yameonyesha kuwa muungano wa vyama ulioundwa na chama tawala cha nchi hiyo Chama cha Kidemokrasia pamoja na vyama vingine, umeshinda katika uchaguzi wa wabunge na serikali za mitaa.

Rais Obiang aliingia madarakani katika mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwaka 1979, na amekuwa rais wa nchi hiyo tangu mwaka  1982.