Rwanda yazindua wiki ya utalii kuchochea ufufukaji wa sekta hiyo
2022-11-28 09:00:42| CRI


 

Shirikisho la Wafanyabiashara wa Utalii nchini Rwanda limezindua toleo la mwaka 2022 la Wiki ya Utalii, ambayo inatarajiwa kuchochea ufufukaji wa sekta hiyo.

Wiki hiyo iliyoanza jumamosi tarehe 26 mwezi huu, inatarajiwa kumalizika Desemba 3, ikiwa na kaulimbiu ya “Kuchukua Hatua za Uvumbuzi Kuchochea Utalii wa Ndani ya Afrika kama injini ya Kufufua Biashara ya Utalii.”

Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho hilo Frank Gisha amesema, Wiki ya Utalii ya Rwanda ni sehemu moja ya mikakati ya kuchochea ufufukaji wa sekta hiyo, na itawawezesha wadau kuonyesha bidhaa zao na kuimarisha uhusiano unaotoa fursa zaidi za kibiashara.

Shughuli mbalimbali zitafanyika katika Wiki hiyo, ikiwemo Wiki ya Migahawa, ambapo watu watapata fursa ya kuonja vyakula vizuri katika migahawa yao kwa bei nafuu.