Umoja wa Mataifa walaani vikali shambulizi la uwanja wa ndege nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
2022-11-28 09:02:20| CRI


 

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulizi lililotokea Alhamis iliyopita dhidi ya askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika uwanja wa ndege wa Obo, ulioko kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati uliosababisha kifo cha askari mmoja wa kulinda amani kutoka Morocco.

Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulizi hilo na kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya askari aliyeuawa na kwa serikali na watu wa Morocco. Amesema mashambulizi kama hayo ni uhalifu wa kivita chini ya sheria ya kimataifa, na kusisitiza kuwa mtu yeyote atakayegundulika kuhusika na kupanga, kuongoza ama kufadhili mashambulizi hayo atachukuliwa hatua kali.