Shambulizi kwenye hoteli mjini Mogadishu lasababisha vifo na majeruhi
2022-11-29 09:08:11| CRI

Polisi wa Somalia wamesema hoteli moja karibu na ikulu mjini Mogadishu imeshambuliwa na watu wenye silaha na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 15 wakiwemo washambuliaji, na wengine wengi walijeruhiwa.

Msemaji wa polisi wa Somalia Bw. Sadiq Dudishe amesema usiku wa tarehe 27 watu wenye silaha walishambulia hoteli ya Villa Rosa karibu na ikulu na kupambana na vikosi vya polisi wa Somalia kwa saa zaidi 20. Tarehe 28 polisi wa Somalia walifanikiwa kudhibiti hoteli na maeneo ya karibu, na kuwaua watu watano wenye silaha na kuwaokoa mateka 60. Shambulizi hilo pia limesababisha vifo vya watu 8 na askari mmoja wa jeshi, na wengine watano walijeruhiwa.

Habari zinasema kundi la al-Shabaab limetangaza kuwajibika na shambulizi hilo na liliwalenga maofisa wa serikali.