WHO yabadilisha jina la homa ya nyani kuwa “mpox” ili kuepusha unyanyapaa
2022-11-29 08:34:32| CRI


 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza kubadilisha jina la homa ya nyani kuwa “mpox” ili kuepusha ubaguzi na unyanyapaa.

Mabadiliko hayo yamekuja baada ya baadhi ya watu na nchi kueleza wasiwasi kwenye mikutano na kuitaka WHO kubadilisha jina la ugonjwa huo.

Mwezi Julai WHO ilitangaza rasmi homa ya nyani ambayo imeenea katika nchi nyingi nje ya Afrika kuwa Dharura ya Kimataifa ya Afya ya Umma (PHEIC), ambayo ni tahadhari ya ngazi ya juu zaidi inayoweza kutolewa na shirika hilo.

Kwa mujibu wa WHO hadi kufikia Jumamosi, nchi 110 zimeripoti maambukizi 81,107 ya homa ya nyani yaliyothibitishwa kimaabara na nyingine 1,526 yanayoshukiwa.