UM waonya dhidi ya kupunguzwa kwa misaada ya chakula kwa wakimibizi nchini Chad kutokana na uhaba wa fedha
2022-11-30 09:04:30| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, amesema Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) yameonya kuwa uhaba wa fedha unaweza kusababisha kupunguzwa kwa misaada ya chakula kwa wakimbizi nchini Chad.

Kwa sasa dola za kimarekani milioni 161 zinahitajika ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ili kukidhi mahitaji ya chakula ya jamii zilizoathirika, ambao ni pamoja na wakimibzi laki 5.19 kutoka Sudan na Afrika ya Kati walioko nchini humo.

Amesema kuanzia mwezi Juni mwaka jana, uhaba mkubwa wa fedha umefanya WFP kutoa nusu tu ya mgao wa chakula kwa wakimbizi na watu wengine walioathiriwa. Lakini mashirika hayo mawili yana wasiwasi kuwa hali yoyote ya kusimamishwa tena kwa misaada ya chakula itaathiri vibaya usalama wa chakula, lishe na ulinzi wa  wakimbizi, haswa wale walio hatarini zaidi.