China yampongeza Obiang kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Guinea ya Ikweta
2022-11-30 08:57:03| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema China inampongeza Bw. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Guinea ya Ikweta, na kuamini kuwa chini ya uongozi wake, ujenzi wa nchi hiyo utapata mafanikio makubwa zaidi.

Bw. Zhao amesema Guinea ya Ikweta ni ndugu na mwenzi mkubwa wa China, nchi hizo mbili zinaaminiana kisiasa kwa  uthabiti, na kudumisha maendeleo ya uhusiano kwenye kiwango cha juu .

Ameongeza kuwa China inazingatia kuendeleza zaidi uhusiano wake na Guinea ya Ikweta, na kupenda kushirikiana na nchi hiyo kuendelea kuzidisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kuhimiza uhusiano wao wa kiwenzi katika pande zote ufikie kiwango cha juu zaidi.