Rais Xi atoa pongezi kwa Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kushikamana na Watu wa Palestina
2022-11-30 11:56:46| cri

Umoja wa Mataifa jana ulifanya Mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kushikamana na Watu wa Palestina, ambapo rais Xi Jinping wa China alitoa pongezi kwa mkutano huo kupitia njia ya simu.

Rais Xi amesema, suala la Palestina siku zote ni kipaumbele cha suala la Mashariki ya Kati. Kutatua suala la Palestina kwa haki na pande zote kunahusiana na utulivu na amani ya kikanda na usawa na haki za kimataifa. Kuishi kwa amani kwa Palestina na Israel na waarabu na wayahudi kushikana mikono kujiendeleza kunalingana na maslahi ya muda mrefu ya pande mbili, ambayo pia ni matarajio ya pamoja ya watu wa nchi mbalimbali. Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kushikilia mpango wa nchi mbili, kulipa kipaumbele suala la Palestina katika ajenda za kimataifa, ili kuwasaidia watu wa Palestina kutimiza ndoto ya kujipatia uhuru na kuanzisha nchi mapema iwezekanavyo.

Rais Xi amesisitiza kuwa, China siku zote inaunga mkono kithabiti shughuli ya haki ya kurejesha uhalali wa taifa ya watu wa Palestina, kuhimiza mazungumzo ya amani na kusukuma mbele amani ya Palestina na Israel. China inaunga mkono kuimarisha mamlaka ya taifa la Palestina, kuunga mkono pande mbalimbali za Palestina kuimarisha umoja, huku ikitaka Palestina na Israel kurudi katika meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo na kuhimiza mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati kurejea katika njia sahihi.