Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-15 chaungana na kituo cha anga ya juu cha China
2022-11-30 08:59:55| CRI

 

Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-15 kimefanikiwa kuungana na kituo cha anga ya juu cha China mapema leo.

Kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA), chombo hicho kilichorushwa Jumanne usiku, kiliungana na moduli ya Tianhe ya Kituo cha Anga ya Juu cha China saa 11 na dakika 42 leo asubuhi.

Wanaanga watatu waliomo kwenye chombo hicho wataingia kwenye moduli ya Tianhe, wenzao watatu wa Shenzhou-14 ambao wamekaa kituoni huko kwa miezi sita wako tayari kukaribisha ujio wao. Hii ni mara ya kwanza kwa wanaanga wa China kushuhudia ujio wa chombo cha anga ya juu wakiwa kituoni.