Aliyekuwa Rais wa China Jiang Zemin amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96
2022-11-30 17:54:01| cri

Aliyekuwa Rais wa China Bw. Jiang Zemin amefariki dunia leo alasiri mjini Shanghai, China akiwa na umri wa miaka 96. Taarifa kutoka vyombo vikuu vya utawala vya China (Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Baraza la serikali, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa, na Kamati kuu ya kijeshi), zinasema Bw. Jiang Zemin ameaga dunia kutokana na saratani ya damu na kushindwa kwa viungo vingi vya mwili, baada ya matibabu yote kushindikana.

Kwenye barua iliyoandikiwa kuuarifu umma wa China kuhusu kifo hicho, Komredi Jiang Zemin ametajwa kuwa alikuwa kiongozi bora aliyeheshimiwa na Chama kizima, jeshi lote na watu wa China wa makabila yote, mfuata nadharia ya u-marx mkuu, mwanamapinduzi mkuu wa tabaka la wafanyakazi, mtawala, mwanamikakati ya kijeshi na mwanadiplomasia, mpiganaji muda wa ukomunisti aliyepitia changamoto, na kiongozi mahiri aliyepigania ujamaa wenye umaalum wa China.

Pia ametajwa kuwa alikuwa nguzo ya uongozi wa pamoja wa kizazi cha tatu cha Chama cha Kikomunisti cha China, na mwanzilishi mkuu wa nadharia ya uwakilishi mtatu.