Uchumi wa Afrika Mashariki wakadiriwa kukua kwa 4.7% mwaka kesho
2022-11-30 09:14:58| CRI

Benki ya maendeleo ya Afrika hivi karibuni ilitangaza ripoti mpya ya makadirio ya mwelekeo wa uchumi wa eneo la Afrika Mashariki kwa mwaka 2022, ikikadiria kuwa ongezeko la uchumi wa eneo hilo kwa mwaka 2023 litafikia asilimia 4.7.

Ripoti hiyo imesema kutokana na kuongezeka kwa bei za nishati na chakula, na kukwama kwa mnyororo wa ugavi duniani, pamoja na athari za majanga ya asili na mfumko wa bei, ongezeko la uchumi wa Afrika Mashariki kwa mwaka huu litapungua na kufikia asilimia 4. Mwaka 2023, uchumi wa eneo hilo unatarajiwa kukua kwa asilimia 4.7, na kufanya Afrika Mashariki kuwa eneo lenye ukuaji mzuri zaidi barani Afrika.