Mwenyekiti wa UNGA asema lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030 "liko nje ya mstari kabisa"
2022-12-01 08:49:59| CRI


 

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) Bw. Csaba Korosi ametoa wito wa kuchukuliwa hatua, kwa kuwa lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030 "liko nje ya mstari kabisa."

Kwenye ujumbe wake kwa Siku ya Ukimwi Duniani ambayo huadhimishwa Desemba 1, Bw. Korosi amesema lengo la kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030 liko nje ya mstari kabisa kutokana na kukosekana kwa usawa, ubaguzi, na kutozingatiwa kwa haki za binadamu.

Bw. Koriso amesema kuna njia ya kisayansi ya kukomesha UKIMWI, lakini cha kusikitisha ni kwamba haipatikani kwa wote. Pia amesema kama jumuiya ya kimataifa itachukua hatua, maambukizi mapya ya VVU milioni 3.6 na vifo milioni 1.7 vinavyohusiana na UKIMWI vitazuiliwa katika muongo huu.