Rais wa mpito wa Chad aeleza nia ya kuimarisha ushirikiano na China katika pande mbalimbali
2022-12-01 08:57:59| CRI

Rais wa mpito wa Chad Mahamat Idriss Deby amesema anatarajia kuimarisha ushirkiano na China katika pande mbalimbali na kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Deby siku hiyo alipopokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa China nchini Chad Wang Xining, alipongeza maendeleo ya uhusiano kati ya Chad na China, na kusisitiza kuwa Chad inathamini urafiki kati ya nchi hizo mbili na ina nia thabiti ya kuendeleza uhusiano na China.

Balozi Wang Xining amesema katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano halisi kati ya nchi hizo mbili umekuwa na mafanikio na China inapenda kuendelea kushirikiana na Chad kukuza uhusiano wao na kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.