Rais Xi Jinping akutana na mwenzake wa Laos Thongloun Sisoulith
2022-12-01 08:29:59| CRI


 

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Laos Thongloun Sisoulith ambaye yuko ziarani nchini China.

Kwenye mazungumzo yao marais hao wamefikia makubaliano mengi kuhusu uhusiano wa nchi zao na ujenzi wa Jumuiya yenye mustakbali wa Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Pia amesema anapenda kushirikiana na mwenzake wa Laos katika kuongoza ujenzi wa Jumuiya yenye mustakbali wa pamoja kati ya China na Laos.

Rais Thongloun Sisoulith amesema China ni nguzo muhimu ya kulinda amani na utulivu wa dunia, kuhimiza maendeleo ya pamoja ya binadamu wote na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja hasa katika wakati huu ambapo mabadiliko makubwa yanashuhudiwa duniani. Amesema anaamini kuwa chini ya uongozi wa Kamati Kuu ya CPC inayoongozwa na Bw. Xi Jinping, kwa uhakika China itatekeleza kikamilifu maazimio ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama, kukamilisha majukumu mbalimbali yaliyowekwa katika mkutano huo na kutimiza lengo la pili la Miaka 100 kama ilivyopangwa. Pia Rais Sisoulith ameishukuru China kwa uungaji mkono wa muda mrefu kwa Laos.

Baada ya mazungumzo, marais hao wawili wameshuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano kati ya vyama na kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo uchumi, biashara, fedha, utamaduni na elimu.