Afrika CDC yataka mifumo thabiti ya afya ya jamii kukabiliana na mzigo wa magonjwa
2022-12-01 08:50:41| CRI


 

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Maradhi cha Afrika (Africa CDC), kimetoa wito wa kuundwa kwa kundi la wafanyakazi wa afya ya jamii wanaofadhiliwa vya kutosha, waliofunzwa na kuhamasishwa ili kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na mzigo unaoongezeka wa magonjwa.

Ofisa mwandamizi wa Africa CDC Bibi Herilinda Temba amesema hayo kwenye warsha iliyofanyika mjini Mombasa, na kusisitiza kuwa uwekezaji katika mfumo thabiti wa afya ya jamii utaongeza uwezo wa bara la kutabiri, kutambua na kutibu magonjwa.

Bibi Temba pia amesema kuajiri wafanyakazi wa ziada wa afya ya jamii pia kutaongeza ufufukaji baada ya janga la UVIKO-19 barani Afrika, ikiashiria kuwa wahudumu wa afya katika jamii wamekuwa wahusika muhimu katika kuongeza uelewa wa kupambana na magonjwa ya kuambukiza kama vile kifua kikuu na VVU/UKIMWI pamoja na kuwasaidia wagonjwa kufuata matumizi ya dawa za muda mrefu.