Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Charles Michel
2022-12-02 09:26:06| CRI

Rais Xi Jinping wa China amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Charles Michel kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing.

Rais Xi ameeleza kuwa China na Ulaya ni nguzo mbili muhimu za kulinda amani ya dunia, ni masoko mawili makubwa yanayokuza maendeleo ya pamoja na pia ni staarabu mbili kuu zinazohimiza maendeleo ya binadamu.

Amesema kuendelea kuimarika kwa uhusiano kati ya China na Ulaya na kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana, kunaenda na maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili na jumuiya ya kimataifa. Umuhimu wa uhusiano huo utajitokeza zaidi wakati dunia ikishuhudia mabadiliko na changamoto kubwa.

Bw. Michel amempongeza Rais Xi kwa kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, pia ametoa salamu za pole kutokana na kifo cha aliyekuwa rais wa China Jiang Zemin. Amesema China haishiriki katika upanuzi wa ardhi na ni mshirika muhimu katika kulinda katiba ya Umoja wa Mataifa na kuunga mkono ushirikiano wa pande nyingi.

Pia amesema Ulaya inapenda kufanya majadiliano na China kuhusu masuala mbalimbali kwenye uhusiano kat yao ili kuzidisha maelewano na kuondoa tofauti.