Viongozi wa Afrika wadhamiria kuharakisha ukuaji wa viwanda barani humo
2022-12-02 09:11:59| CRI


 

Viongozi wa Afrika wamedhamiria kwa "maamuzi madhubuti na yenye maono ya mbali" kuharakisha ukuaji wa viwanda, kufanya uchumi uwe na vyanzo mbalimbali na kuhimiza biashara.

Taarifa iliyotolewa jana na Umoja wa Afrika (AU) kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Viwanda na Mseto wa Kiuchumi uliofanyika wiki iliyopita nchini Niger, viongozi hao wamesisitiza kuongeza kasi ya ukuaji wa viwanda na kufanya uchumi uwe na vyanzo mbalimbali, huku vipaumbele vikiwa kwenye afya na dawa, magari, madini, chakula na lishe, na nguo ili kupunguza utegemezi kutoka nje.

Wamesisitiza zaidi haja ya kuongeza uwekezaji katika miundombinu na nishati kwa msaada wa taasisi za fedha na washirika, ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ushindani wa uchumi wa Afrika.